Al-Kahf 18:29
الكهفوَقُلِ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَن شَآءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَآءَ فَلْيَكْفُرْ ۚ إِنَّآ أَعْتَدْنَا لِلظَّـٰلِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمْ سُرَادِقُهَا ۚ وَإِن يَسْتَغِيثُوا۟ يُغَاثُوا۟ بِمَآءٍ كَٱلْمُهْلِ يَشْوِى ٱلْوُجُوهَ ۚ بِئْسَ ٱلشَّرَابُ وَسَآءَتْ مُرْتَفَقًا
Na sema: Hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akufuru. Hakika Sisi tumewaandalia madhalimu Moto ambao kuta zake zitawazingira. Na wakiomba msaada, watasaidiwa kwa kupewa maji yaliyo kama mafuta yaliyotibuka, yatakayowababua nyuso zao. Ni kinywaji kiovu mno kilichoje hicho, na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia palipoje hapo!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae. Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu Moto ambao utawazunguka kama khema. Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka. Yatayo wababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno! [29]
[29] Sema ewe Mtume!: Hakika haya niliyo kuja nayo ni kweli tupu iliyo toka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye taka kuyaamini na ayaamini. Kwani hiyo ni kheri yake mwenyewe. Na anaye taka kuyakataa na akatae. Kwani huyo haidhulumu ila nafsi yake mwenyewe. Hakika Sisi tumekwisha muwekea tayari anaye jidhulumu nafsi yake kwa ukafiri Moto utao mzunguka kama khema. Na hao walio dhulumu wakiomba wasaidiwe kwa maji huko katika Jahannamu, wataletewa maji kama mafuta yaliyo tibuka yamoto mno, hubabua nyuso kwa uvukuto wake! Kinywaji hicho ni kibaya mno, na Jahannamu ni pahali paovu pa mapumziko yao!!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na useme kuwaambia hawa walioghafilika, Haya niliyowaletea ndio ukweli utokao kwa Mola wenu. Basi yoyote kati yenu atakaye kuamini na akafanya matendo yanayolingana na hiyo Imani, na afanye kwani hilo ni bora kwake, na mwenye kutaka kukanusha na akanushe kwani atakua hakumdhulumu yoyote isipokuwa nafsi yake mwenyewe. Hakika sisi tumewatayarishia makafiri Moto mkali ambao kuta lake limewazunguka. Na makafiri hawa wakitaka msaada Motoni wapatiwe maji kwa vile kiu ilivyo kali, wataletewa maji kama mafuta machafu yaliyo moto sana yanayochoma nyuso zao. Ni kibaya kilioje kinywaji hiki ambacho hakiondoi kiu yao bali kinaizidisha na ni ubaya ulioje wa Moto kuwa ndio mashukio yao na makazi. Katika haya pana onyo na tishio kali kwa yoyote mwenye kuipa mgongo haki na asiuamini utume wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na asifanye vitendo vinavyolingana na Imani hiyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net