Al-Kahf 18:28
الكهفوَٱصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِٱلْغَدَوٰةِ وَٱلْعَشِىِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُۥ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُۥ عَن ذِكْرِنَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ وَكَانَ أَمْرُهُۥ فُرُطًا
Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka uso wake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake, na mambo yake yakawa ni kupita tu mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usimt'ii tuliye mghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake yakawa yamepita mpaka. [28]
[28] Ewe Mtume! Shikamana na usuhuba wa masahaba wako Waumini, wanao muabudu Mwenyezi Mungu peke yake asubuhi na jioni daima, huku wanataka radhi zake. Wala jicho lako lisiwawache hao kuwaangalia wapinzani wa kikafiri kwa kutaka kustarehe nao katika mapambo ya maisha ya dunia. Wala usikubali kuwafukuza Waumini mafakiri katika baraza yako kwa kumridhisha huyo tuliye mghafilisha moyo wake na kutukumbuka Sisi, kwa kuwa yeye mwenyewe hakuwa tayari kwa hayo, na akawa ni mtumwa wa pumbao lake, na mambo yake katika vitendo vyake vyote hayakufuata njia iliyo sawa. Na anapo katazwa Nabii, basi ndio wanakatazwa wengineo (yaani sote sisi). Na hakika Nabii s.a.w. hataki maisha ya dunia na pumbao lake. Lakini makatazo hayo anaelekezewa Nabii ili wenginewe watahadhari na kutaka pumbao la dunia. Kwani ikiwa yaweza kuwa kwake kutaka pumbao la kimwili, basi kila mwanaadamu yaweza kuwa katika nafsi yake. Kwa hivyo ajilinde.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na uvumilie nafsi yako, ewe Mtume, pamoja na maswahaba wako miongoni mwa Waumini masikini wanaomuabudu Mola wao Peke Yake na kumuomba Yeye kucha na kutwa, wakiomba kupata radhi Zake, ukae pamoja nao na utangamane nao, na usiuepushe uso wako na wao kuwaangalia wasiokuwa wao miongoni mwa makafiri kwa kutaka kujistarahesha na pambo la uhai wa kilimwengu. Na usimtii yule tulioufanya moyo wake ughafilike kututaja na akafadhilisha kufuata matamanio yake juu ya kumtii Mola Wake na mambo yake yakawa, katika matendo yake yote, yamepotea na kuangamia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net