Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 27

Al-Kahf 18:27

الكهف

وَٱتْلُ مَآ أُوحِىَ إِلَيْكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَ ۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَـٰتِهِۦ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلْتَحَدًا

Maana

Na soma yale uliyofunuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hakuna yeyote awezaye kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio yoyote isipokuwa kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na soma uliyo funuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hapana wa kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio isipo kuwa kwake. [27]

[27] Ewe Mtume! Soma uliyo funuliwa kwa wahyi katika Qur'ani. Na katika hayo yamo uliyo funuliwa ya khabari za hao vijana. Wala usisikilize hayo maskhara yao ya kutaka ubadilishe muujiza wa Qur'ani kwa muujiza mwingine. Kwani hakika hapana wa kuyageuza anayo simulia Mwenyezi Mungu maneno ya haki katika miujiza yake. Hakika hapana awezae kubadilisha hayo. Wala usende kinyume na amri ya Mola wako Mlezi, kwani hapo tena hutapata wa kumkimbilia kukuhifadhi naye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na usome Qur’ani, ewe Mtume, ambayo Allah Mtukufu Amekuletea wahyi nayo, kwani hiyo Qur’ani ni Kitabu ambacho hakuna mwenye kuyageuza maneno yake kwa kuwa ni ya kweli na ya uadilifu, na hutapata isipokuwa kwa Mola wako mahala pa wewe kuhamia wala pa kujilinda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net