Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 26

Al-Kahf 18:26

الكهف

قُلِ ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثُوا۟ ۖ لَهُۥ غَيْبُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ أَبْصِرْ بِهِۦ وَأَسْمِعْ ۚ مَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِىٍّ وَلَا يُشْرِكُ فِى حُكْمِهِۦٓ أَحَدًا

Maana

Sema: Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi muda waliokaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi. Kuona vyema kulikoje kwake na kusikia kuzuri kulikoje! Hawana mlinzi yeyote isipokuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi muda walio kaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi. Kuona kulioje na kusikia kwake! Hawana mlinzi isipo kuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake. [26]

[26] Ewe Mtume! Waambie watu: Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kujua zama zao zote. Kwani Yeye Subhanahu ndiye aliye khusika kujua siri za mbingu na ardhi. Jinsi gani kulivyo tukuka kuona kwake kwa viumbe vyote! Na jinsi gani kulivyo tukuka kusikia kwake kwa kila cha kusikilizana! Na hapana katika wa mbinguni na wa katika ardhi wa kuendesha mambo yao isipo kuwa Yeye. Na wala hapana wa kumshiriki katika hukumu yake kiumbe chochote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ukiulizwa, ewe Mtume, kuhusu muda wa kukaa kwao kwenye pango, na wewe huna ujuzi wa hilo na hukupata wahyi kutoka kwa Allah Mtukufu, basi usiongee lolote kuhusu jambo hilo, isipokuwa sema, «Allah Mtukufu Ndiye Mjuzi zaidi wa muda wa kukaa kwao. Ni wake Yeye ujuzi wa visivyoonekana vya mbinguni na ardhini, ni kuona kulioje Kwake na kusikia kulioje!» Yaani : uonee ajabu ukamilifu wa kuona Kwake na wa kusikia Kwake na wa kukizunguka Kwake kila kitu. Viumbe hawana yoyote mwingine isipokuwa Yeye wa kusimamia mambo yao, na Hana mshirika katika uamuzi Wake, hukumu Yake na sheria Zake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net