Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 22

Al-Kahf 18:22

الكهف

سَيَقُولُونَ ثَلَـٰثَةٌ رَّابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًۢا بِٱلْغَيْبِ ۖ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ ۚ قُل رَّبِّىٓ أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ ۗ فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَآءً ظَـٰهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِم مِّنْهُمْ أَحَدًا

Maana

Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: “Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao.ˮ Wanabahatisha ghaibu. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: “Mola wangu Mlezi ndiye anayejua sawa sawa hesabu yao. Hawawajui isipokuwa wachache tu.ˮ Basi usibishane juu yao isipokuwa kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize habari zao kwa yeyote yule miongoni mwao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao. Wanavurumisha ovyo. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye jua sawa sawa hisabu yao. Hawawajui ila wachache tu. Basi usibishane juu yao ila kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize khabari zao kwa yeyote yule. [22]

[22] Watasema kikundi fulani katika Watu wa Kitabu (Biblia) wanao jiingiza katika mzozano wa kisa cha Ahlil Kahf (Watu wa Pangoni) kwamba hao walikuwa watatu na wa nne wao ni mbwa wao. Na wengine wanasema: Walikuwa watano, na wa sita wao ni mbwa wao. Tena wengine wanasema: Wao ni saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Waambie hawa wanao khitalifiana: Mola wangu Mlezi ni Mjuzi ambaye hapana wa kumshinda ujuzi wake kuijua idadi yao. Wala hapana wajuao ila watu wachache tu ambao Mwenyezi Mungu amewajuvya hisabu yao. Basi wewe usijadiliane na hao wanao khitalifiana juu ya mas-ala ya hao vijana, ila majadiliano ya juu juu ya upole, bila ya kujaribu kuwakinaisha. Kwani wao hawakinaiki. Wala msimuulize yeyote kati yao juu ya khabari zao. Wewe hakika imekwisha kujia iliyo kweli isiyo na shaka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watasema baadhi ya Watu wa Kitabu wenye kujishughulisha na mambo yao kwamba wao ni watatu na wa nne wao ni mbwa wao, na kundi lingine litasema kwamba wao ni watano na wa sita wao ni mbwa wao. Maneno ya makundi mawili haya ni maneno ya kudhania bila dalili yoyote. Na kundi la tatu litasema kwamba wao ni saba na wa nane wao ni mbwa wao. Sema, ewe Mtume, «Mola wangu Ndiye Mjuzi kabisa wa idadi yao,» hakuna anayeijua idadi yao isipokuwa ni wachache kati ya viumbe Wake. Basi usibishane na Watu wa Kitabu kuhusu idadi yao isipokuwa ubishi wa juu juu usiokuwa na undani kwa kuwasimulia yale ambayo Allah Mtukufu amekuletea wahyi nayo, na usiulize kuhusu idadi yao na hali zao, kwani wao hawalijui hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net