Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 21

Al-Kahf 18:21

الكهف

وَكَذَٰلِكَ أَعْثَرْنَا عَلَيْهِمْ لِيَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ لَا رَيْبَ فِيهَآ إِذْ يَتَنَـٰزَعُونَ بَيْنَهُمْ أَمْرَهُمْ ۖ فَقَالُوا۟ ٱبْنُوا۟ عَلَيْهِم بُنْيَـٰنًا ۖ رَّبُّهُمْ أَعْلَمُ بِهِمْ ۚ قَالَ ٱلَّذِينَ غَلَبُوا۟ عَلَىٰٓ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِم مَّسْجِدًا

Maana

Na namna hivo ndivyo tulivyowajulisha kwa watu ili wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipokuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao, wakasema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema wale walioshinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutajenga msikiti juu yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipo kuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao walisema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema walio shinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti juu yao. [21]

[21] Na kama tulivyo walaza na tukawaamsha tulikuja watambulisha kwa watu wa ule mji wapate kujua kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kufufua wafu ni ya kweli. Na Kiyama hapana shaka kitakuja. Watu wa ule mji wakamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Kisha Mwenyezi Mungu akawafisha wale vijana. Watu sasa wakazozana kwa mintarafu yao. Baadhi yao wakasema: Jengeni jengo kwenye mlango wa pango, na tuwaache wao na shani yao. Kwani Mola wao Mlezi anaijua vyema hali yao. Na wakasema wenye kusikilizwa miongoni mwao: Hapa pahala pao tutafanya msikiti kwa sababu ya ibada.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama vile tulivyowalaza miaka mingi na tukawaamsha baada yake, tuliwafanya wajulikane na watu wa zama hizo baada ya muuzaji kuzigundua aina ya dirhamu alizozileta yule aliyetumwa na wao, ili watu wapate kujua kwamba ahadi ya Allah Mtukufu ya Ufufuzi ni kweli na kwamba Kiyama hakina shaka ni chenye kuja. Kutahamaki hao waliowagundua watu wa Pango wakawa ni wenye kushindana kuhusu jambo la Kiyama: kuna waliolikubali na kuna waliolipinga. Na Allah Mtukufu Akajaalia kule kuwagundua watu wa Pango ni hoja kwa Waumini juu ya makafiri. Na baada ya mambo yao kugunduliwa na wakafa, lilisema kundi moja la wale waliowagundua, «Jengeni kwenye mlango wa pango jengo la kuwasitiri kisha muwawache na mambo yao, Allah Mtukufu ni Mjuzi wa hali yao.» Na wakasema wale wenye kusikilizwa maneno yao na wenye uwezo miongoni mwao, «Tutatengeneza mahali pao hapo msikiti wa kufanya ibada.» Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, alikataza kuyafanya makaburi ya Manabii na watu wema kuwa misikiti, na alimlaani mwenye kufanya hivyo katika nyasia zake za mwisho kwa umati wake. Pia alikataza kabisa kujenga juu ya makaburi na kuyajengea na kuandika juu yake, kwani yote hayo ni miongoni mwa upitaji kiasi unaopelekea kuwaabudu waliomo ndani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net