Al-Kahf 18:20
الكهفإِنَّهُمْ إِن يَظْهَرُوا۟ عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِى مِلَّتِهِمْ وَلَن تُفْلِحُوٓا۟ إِذًا أَبَدًا
Kwani wao wakiwatambua, watawapiga mawe, au watawarudisha katika dini yao, na hapo kamwe hamtafanikiwa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani wao wakikutambueni watakupigeni mawe, au watakurudisheni katika dini yao; na hapo hamtafanikiwa kabisa! [20]
[20] Kwani hao watu wakikuoneni watakuuweni kwa kukupopoeni mawe, au watakurejesheeni katika ukafiri kwa nguvu. Nanyi mkirejea ukafirini basi hamtaongokewa kabisa duniani wala Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika watu wenu wakiwagundua mlipo watawapiga mawe wawaue au watawarudisha kwenye dini yao muwe makafiri, na mkifanya hivyo basi hamtafaulu kabisa kupata matakwa yenu ya kuingia Peponi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net