Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 19

Al-Kahf 18:19

الكهف

وَكَذَٰلِكَ بَعَثْنَـٰهُمْ لِيَتَسَآءَلُوا۟ بَيْنَهُمْ ۚ قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ كَمْ لَبِثْتُمْ ۖ قَالُوا۟ لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۚ قَالُوا۟ رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثْتُمْ فَٱبْعَثُوٓا۟ أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمْ هَـٰذِهِۦٓ إِلَى ٱلْمَدِينَةِ فَلْيَنظُرْ أَيُّهَآ أَزْكَىٰ طَعَامًا فَلْيَأْتِكُم بِرِزْقٍ مِّنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا

Maana

Na kwa namna hiyo tuliwainua usingizini ili wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi muda mliokaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu aende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa awaletee cha kula. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala kamwe asiwataje kwa yeyote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi anajua zaidi muda mlio kaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu ende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa akuleteeni cha kukila. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala asikutajeni kabisa kwa yeyote. [19]

[19] Kama tulivyo walaza tuliwaamsha wapate kuulizana wenyewe kwa wenyewe wamelala muda gani? Mmoja wao akasema: Umekupitieni muda gani katika usingizi? Wakasema: Tumelala muda wa siku au baadhi ya siku. Walivyo kuwa hawana yakini nayo hayo wakasema: Mwachieni mambo haya Mwenyezi Mungu; kwani Yeye ni Mjuzi zaidi wa haya. Na ende mmoja wenu mjini, na achukue hizi sarafu za fedha achague chakula kizuri kabisa akuleteeni mle. Na awe na mafahamiano mema. Wala mambo yenu yasijuulikane na mtu yeyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama tulivyowalaza na tukawahifadhi muda huu mrefu, tuliwaamsha kutoka kwenye usingizi wao kama vile walivyokuwa bila kubadilika, ili waulizane wao kwa wao, «Ni muda gani tulikaa tukiwa tumelala hapa?» Baadhi yao wakasema, «Tumekaa siku moja au sehemu ya siku.» Na wengine ambao mambo yaliwachanganyikia walisema, «utegemezeni ujuzi wa hilo kwa Allah Mtukufu, kwani Mola wenu ni Mjuzi zaidi wa kipindi mlichokikaa, basi mtumeni mmoja wenu na pesa zenu hizi za fedha aende mjini kwetu aangalie ni mtu gani hapo mjini mwenye chakula kizuri zaidi na cha halali, na awaletee chakula kutoka kwake, na ajifichefiche akiwa na muuzaji katika kununua kwake ili tusigundulike na mambo yetu yakafichuka, na msijulikane kabisa na mtu yoyote».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net