Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 14

Al-Kahf 18:14

الكهف

وَرَبَطْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ إِذْ قَامُوا۟ فَقَالُوا۟ رَبُّنَا رَبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ لَن نَّدْعُوَا۟ مِن دُونِهِۦٓ إِلَـٰهًا ۖ لَّقَدْ قُلْنَآ إِذًا شَطَطًا

Maana

Na tukazitia nguvu nyoyo zao waliposimama na wakasema, "Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Kamwe hatutamuomba mwingine badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo, itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na wakasema: Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita mwenginewe kabisa badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka. [14]

[14] Na tulizithibitisha nyoyo zao juu ya Imani na subira ya kuvumilia shida, pale walipo simama mbele ya watu wao wakasema kwa kujifunga kwa ahadi: Ewe Mola wetu Mlezi! Wewe ndiye wa Haki, Mola Mlezi wa mbingu na ardhi! Sisi hatumuabudu mungu mwenginewe. Wala hatutoiwacha itikadi hii. Wallahi! Tukisema jenginelo basi itakuwa tunasema lilio mbali kabisa na kweli!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tukazipa nguvu nyoyo zao kwa Imani na tukazikaza nia zao kwa hiyo Imani, waliposimama mbele ya mfalme kafiri, huku naye akiwalaumu kwa kuacha ibada ya masanamu, na wakamwambia, «Mola wetu tunayemuabudu ni Mola wa mbingu na ardhi, hatutaabudu waungu wengine, na tukisema lingine lisilokuwa hili tutakuwa tumesema neno la udhalimu lililo mbali na haki».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net