Al-Kahf 18:15
الكهفهَـٰٓؤُلَآءِ قَوْمُنَا ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً ۖ لَّوْلَا يَأْتُونَ عَلَيْهِم بِسُلْطَـٰنٍۭ بَيِّنٍ ۖ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا
Hawa kaumu yetu walijifanyia miungu mingine badala yake Yeye. Kwa nini basi hawawatolei uthibitisho ulio dhahiri? Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawa watu wetu wameshika miungu mingine badala yake Yeye. Kwa nini basi hawawatolei uthibitisho ulio dhaahiri? Na nani aliye dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu? [15]
[15] Kisha wakaambiana wenyewe kwa wenyewe: Hawa watu wetu wamemshirikisha Mwenyezi Mungu. Lau kuwa wameleta hoja iliyo wazi ya kuthibitisha ungu wa hivyo wanavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Hakika watu hawa ni wenye kudhulumu kwa vitendo vyao hivyo. Wala hapana aliye zidi udhaalimu kuliko mwenye kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo kwa kumsingizia washirika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha wakaambiana wao kwa wao, Watu wetu hawa wamewachukua wasiokuwa Allah Mtukufu wakawafanya ni waungu, basi si watuletee ushahidi waziwazi kuwa hao wafaa kuabudiwa? Hakuna yoyote aliye dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah Mtukufu urongo kwa kudai kuwa Ana mshirika katika kuabudiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net