Al-Kahf 18:13
الكهفنَّحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُم بِٱلْحَقِّ ۚ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ ءَامَنُوا۟ بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَـٰهُمْ هُدًى
Sisi tunakusimulia habari zao kwa haki. Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uongofu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu. [13]
[13] Ewe Mtume! Sisi tunakusimulia khabari zao kweli kweli: Hakika hao walikuwa vijana katika zama zilizo pita ambao walikuwa wameshika Dini ya Haki. Walimuamini Mola wao Mlezi kuwa ni Mmoja tu, na ilihali wamezungukwa na washirikina.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tunakuhadithia, ewe Mtume, habari yao kwa ukweli. Watu wa pango ni vijana waliomuamini Mola wao na wakafuata amri Zake, na tukawazidishia uongofu na uimara katika haki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net