Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 12

Al-Kahf 18:12

الكهف

ثُمَّ بَعَثْنَـٰهُمْ لِنَعْلَمَ أَىُّ ٱلْحِزْبَيْنِ أَحْصَىٰ لِمَا لَبِثُوٓا۟ أَمَدًا

Maana

Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili yale ndilo lilihesabu sawa zaidi urefu wa muda waliokaa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili lilio hisabu sawa muda walio kaa. [12]

[12] Kisha Mwenyezi Mungu aliwaamsha baada ya kulala kwa muda mrefu, ili matokeo yake yawe ni kudhihirisha ujuzi wetu ni nani katika makundi mawili aliye sibu kukisia muda wa kulala kwao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawaamsha kutoka kwenye usingizi wao ili tuwaonyeshe watu tuliyoyajua hapo kale ipate kupambanuka ni lipi kati ya makundi mawili, yanayobishana juu ya kipindi cha kukaa kwao, limedhibiti zaidi katika kuhesabu: je, walikaa siku moja au mbili au walikaa muda mrefu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net