Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 105

Al-Kahf 18:105

الكهف

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِمْ وَلِقَآئِهِۦ فَحَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ وَزْنًا

Maana

Hao ni wale waliozikufuru Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo matendo yao yakapotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawasimamishia mizani yoyote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ni wale walio zikanusha Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimepotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawathamini kitu. [105]

[105] Hao ndio walio zikataa dalili za uwezo wa Mwenyezi Mungu, na wakaikanusha Siku ya kufufuliwa na kuhisabiwa. Basi vitendo vyao vimepotea bure, na Siku ya Kiyama watastahiki kudharauliwa na kupuuzwa, kwani hawana a'mali ya kutiwa maanani!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio waliopata hasara zaidi kivitendo, ndio wao waliozikataa aya za Mola wao na wakazikanusha na wakapinga kuwa watakutana na Yeye Siku ya Kiyama, hivyo basi matendo yao yakabatilika kwa sababu ya ukafiri wao na kwa hivyo hatutawajali chochote Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net