Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 106

Al-Kahf 18:106

الكهف

ذَٰلِكَ جَزَآؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا۟ وَٱتَّخَذُوٓا۟ ءَايَـٰتِى وَرُسُلِى هُزُوًا

Maana

Hayo ndiyo malipo yao, Jahannam, kwa walivyokufuru na wakafanyia stihizai Ishara zangu na Mitume wangu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hiyo Jahannamu ni malipo yao kwa walivyo kufuru na wakafanyia kejeli Ishara zangu na Mitume wangu. [106]

[106] Hayo ndiyo tuliyo yabainisha na tukayapambanua, hali ya hawa; na malipo yao kwa hayo ni Jahannamu kwa sababu ya kufuru zao na kuzifanyia maskhara Ishara za Mwenyezi Mungu alizo ziteremsha, na Mitume alio watuma.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Malipo hayo waliyoandaliwa kwa kubatilika matendo yao, ni moto wa Jahanamu, kwa sababu ya kumkanusha kwao Allah Mtukufu na kuzifanyia kwao shere na mchezo aya Zake na hoja za Mitume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net