Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 104

Al-Kahf 18:104

الكهف

ٱلَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

Maana

Ni wale ambao juhudi yao katika uhai wa dunia ilipotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya matendo mazuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri. [104]

[104] Ni hao vilio haribika vitendo vyao katika maisha ya duniani kwa kuharibika itikadi yao, na hali wao wanaitakidi kuwa ndio wanafanya vitendo vyema!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wao ni wale ambao matendo yao yalipotea katika maisha ya ulimwengu- nao ni washirikina wa watu wako na wengineo kati ya wale waliopotea njia ya sawa wasiwe kwenye uongofu wala usawa- na hali wao wanadhania kuwa wanayatengeneza matendo yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net