Al-Kahf 18:103
الكهفقُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِٱلْأَخْسَرِينَ أَعْمَـٰلًا
Sema: Je, tuwatajieni wenye hasara mno katika vitendo vyao?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao?. [103]
[103] Ewe Mtume! Waambie hawa makafiri: Je, nikutajieni watu watao pata khasara mno kwa vitendo vyao na watao kosa thawabu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie watu, ewe Mtume, kwa kuwaonya: Je, tuwapashe habari ya watu wenye vitendo vya hasara zaidi?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net