Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 102

Al-Kahf 18:102

الكهف

أَفَحَسِبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَن يَتَّخِذُوا۟ عِبَادِى مِن دُونِىٓ أَوْلِيَآءَ ۚ إِنَّآ أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَـٰفِرِينَ نُزُلًا

Maana

Je, wanadhani wale waliokufuru kwamba watawafanya waja wangu kuwa vipenzi wao badala yangu Mimi? Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo pahali pa kuteremkia pa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, wanadhani walio kufuru ndio wawafanye waja wangu ndio walinzi wao badala yangu Mimi? Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo mahala pa kuteremkia makafiri. [102]

[102] Je, macho ya makafiri yamepofuka hata wakadhani kwamba kuwafanya watumwa wangu, Malaika na Isa, kuwa ni miungu, wakiwaabudu badala yangu Mimi, kutawapa manufaa na kuwakinga na adhabu? Hakika Sisi tumewaandalia Jahannamu ndio pahali pao pa kukaa wapate huko malipo wanayo yastahiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, walidhani walionikanusha kuwa watawafanya waja wangu kuwa ni waungu badala yangu, wawe ni wategemewa wao? Kwa hakika tumewatayarishia wenye kukanusha moto wa Jahanamu uwe ndio mashukio yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net