Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 101

Al-Kahf 18:101

الكهف

ٱلَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِى غِطَآءٍ عَن ذِكْرِى وَكَانُوا۟ لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا

Maana

Wale ambao macho yao yalikuwa paziani hawanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao kwamba macho yao yalikuwa paziani hayanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia. [101]

[101] Na hayo ni kwa kuwa macho yao walipo kuwa duniani yalikuwa yameghafilika hayaoni Ishara za Mwenyezi Mungu kama kwamba yamezibwa na pazia; na walikuwa kwa upotovu wao hawawezi kusikia Wito wa Haki, kama mtu aliye kuwa kiziwi. "Wale ambao kwamba macho yao yalikuwa paziani hayanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia": Ni wale ambao macho yao yameghafilika na kunizingatia Mimi katika mbingu na ardhi. Na kwa hivyo hii Aya tukufu inazindua watu wazingatie yote yalio wazunguka yanayo onyesha Ishara za kuwepo Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao macho yao ulimwenguni yalikuwa yamefunikwa na kutonikumbuka, hayazioni dalili zangu, na walikuwa hawawezi kustahamili kuzisikia hoja zangu zenye kupelekea kuniamini mimi na Mtume wangu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net