Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 18 · Aya ya 1

Al-Kahf 18:1

الكهف

ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ ٱلْكِتَـٰبَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُۥ عِوَجَا ۜ

Maana

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye alimteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kuwa na upogo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye amemteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kina upogo. [1]

[1] Kuhimidiwa, yaani kusifiwa na kushukuriwa kwa wema, anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambaye amemteremshia mja wake, Muhammad, hii Qur'ani. Na wala hakujaalia kuwa ndani yake kipo chochote cha dosari, kilicho kwenda kombo na kuacha usawa. Bali ndani yake mna Haki tupu, isiyo na shaka yoyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sifa njema zote ni za Allah Mtukufu, kwa kuwa Ana sifa ambazo zote ni sifa za ukamilifu na kwa kuwa ana neema zilizo wazi na zilizofichika, za kidini na za kidunia, Ambaye Alifanya wema Akamteremshia mja Wake na Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), Qur’ani na hakuifanya kuwa na kitu chochote cha kupotoka na haki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Kahf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net