Al-Kahf 18:2
الكهفقَيِّمًا لِّيُنذِرَ بَأْسًا شَدِيدًا مِّن لَّدُنْهُ وَيُبَشِّرَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعْمَلُونَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا حَسَنًا
Kimenyooka sawa sawa, ili kionye adhabu kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba hakika wana ujira mzuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kimenyooka sawa, ili kitoe onyo kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba watapata ujira mzuri. [2]
[2] Na Mwenyezi Mungu ameijaalia Qur'ani imesimama, imenyooka sawa sawa katika mafunzo yake ili kuwaonya wanao kufuru na kukataa, kuwa watapata adhabu kali itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na iwape bishara njema wanao isadiki, ambao wanatenda vitendo vyema, ya kwamba watapata malipo mazuri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Ameifanya kuwa ni Kitabu kilichonyooka kisicho na tafauti ndani yake wala mgongano, ili Awaonye makafiri na adhabu kali itokayo Kwake, na Awape bishara njema wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake wanaofanya matendo mema, kwamba wao watakuwa na malipo mengi, nayo ni Pepo,
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net