Al-Israa 17:111
الإسراءوَقُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٌ فِى ٱلْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُۥ وَلِىٌّ مِّنَ ٱلذُّلِّ ۖ وَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًۢا
Na sema: Alhamdulillah (sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) ambaye hakujifanyia mwana yeyote, wala hana mshirika yeyote katika ufalme, wala hana mlinzi yeyote wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na sema: Alhamdulillah, Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa. [111]
[111] Nasema Alhamdulillah, Himdi zote, yaani sifa na shukrani, ni za Mwenyezi Mungu ambaye hakuzaa mwana, kwani hamhitajii; wala hana mshirika katika ufalme, kwani Yeye peke yake ndiye aliye uanzisha; wala hana msaidizi wa kumtia nguvu kwa udhaifu fulani unao mpata. Na mtukuze Mola wako Mlezi kwa utukufu mkubwa ulio laiki naye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na useme, «Shukrani zote ni za Allah Mtukufu, ukamilifu na sifa njema ni Zake, Aliyetakasika na mwana na mshirika katika uungu Wake. Na Allah Mtukufu Hana msaidizi yoyote kati ya viumbe vyake, Yeye Ndiye Mkwasi na Ndiye Mwenye nguvu, na wao ndio mafukara wanaomhitajia.» Na umtukuze matukuzo yaliyotimia, kwa kumsifu, kumuabudu Peke Yake bila ya mshirika, na kumtakasia Dini yote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net