Al-Israa 17:110
الإسراءقُلِ ٱدْعُوا۟ ٱللَّهَ أَوِ ٱدْعُوا۟ ٱلرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا۟ فَلَهُ ٱلْأَسْمَآءُ ٱلْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَٱبْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا
Sema, "Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Ar-Rahman (Mwingi wa rehema), kwa jina lolote mnalomwita. Hakika, Yeye ana majina mazuri zaidi." Wala usiswali Swala yako kwa sauti kubwa sana, wala usiifiche kwa sauti ndogo sana, bali shika njia ya kati na kati ya hizo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usitangaze Swala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo. [110]
[110] Waambie hawa washirikina: Mwiteni Mwenyezi Mungu kwa jina la Allah, au jina la Rahman; kwani jina lolote mtalo mwitia ni zuri. Yeye Mtukufu ana majina mengi mazuri mazuri. Wala hamdanganyikiwi kwa kutumia majina mengi kuwa kwa hivyo mwenye kuitwa ni zaidi ya Mmoja. Na unapo soma Qur'ani katika Swala zako, basi usipaze sauti yako wakasikia washirikina wakakusibabi na wakakuudhi. Wala usifanye kwa siri hata Waumini wakawa hawasikii. Kuwa kati kati katika kusoma kwako.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina wa watu wako waliokupinga kutumia kwako neno la Yã Allãh, Yã Raḥmãn, katika maombi, «Muombeni Allãh (Allah Mtukufu) au muombeni Raḥmãn (Mwingi wa rehema), kwani kwa majina yoyote yake mkimuomba huwa mnamuomba Mola Mmoja, kwa kuwa majina Yake yote ni mazuri. Wala usidhihirishe kisomo katika Swala yako wakakusikia washirikina, wala usisome kwa siri wasikusikie maswahaba zako, na uwe kati na kati baina ya kudhihirisha na kusirisha».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net