Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 109

Al-Israa 17:109

الإسراء

وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩

Maana

Na huanguka kifudifudi na huku wanalia, na inawazidisha unyenyekevu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na huanguka kifudifudi na huku wanalia, na inawazidisha unyenyekevu. [109]

[109] Na huangukia tena kwenye nyuso zao mara ya pili wakilia kwa kumkhofu Mwenyezi Mungu, na Qur'ani inawazidisha unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hapo hawa wanaporomoka hali ya kusujudu kwa nyuso zao, huku wakilia kwa kuathirika na mawaidha ya Qur’ani. Na kule kuisikia Qur’ani na mawaidha yake kunawafanya wazidi kuinyenyekea amri ya Allah Mtukufu na kuunyenyekea uwezo Wake mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net