Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 99

Al-Israa 17:99

الإسراء

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَّا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى ٱلظَّـٰلِمُونَ إِلَّا كُفُورًا

Maana

Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhalimu walikataa isipokuwa kukufuru tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhaalimu hawataki ila ukafiri. [99]

[99] Jee wameghafilika na hawakujua kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, juu ya ukubwa wao, ni Mwenye kuweza kuumba watu na majini kama wao? Na Mwenye kuweza hayo, vipi awe hawezi kuwarejesha wao upya, na hilo ni jepesi zaidi kwake! Na Yeye Subhanahu ameweka muda maalumu wa kuwarejesha tena baada ya kwisha kufa, na huo hauna shaka kuwa. Na muda huo ndio Siku ya Kiyama. Na juu ya hivyo walio zidhulumu nafsi zao kwa ukafiri wanakataa baada ya kuletewa hoja hizi. Na hayo si kwa lolote ila kwa ukafiri tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, kwani wameghafilika hawa washirikina, wasiangalie na kujua kwamba Allah Mtukufu, Aliyeumba mbingu na ardhi na viumbe vilivyomo ndani yake bila ya mfano uliotangulia, ni muweza wa kuumba mfano wao baada ya kumalizika kwao? Allah Mtukufu amewawekea washirikina hawa wakati maalumu wa kufa kwao na kuadhibiwa, hapana shaka wakati huo utawafikia. Na pamoja na uwazi wa haki na dalili Zake walikataa washirikina isipokuwa kuikanusha Dini ya Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net