Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 100

Al-Israa 17:100

الإسراء

قُل لَّوْ أَنتُمْ تَمْلِكُونَ خَزَآئِنَ رَحْمَةِ رَبِّىٓ إِذًا لَّأَمْسَكْتُمْ خَشْيَةَ ٱلْإِنفَاقِ ۚ وَكَانَ ٱلْإِنسَـٰنُ قَتُورًا

Maana

Sema, "Lau kuwa nyinyi mnazimiliki hazina za rehema za Mola wangu Mlezi, basi hapana shaka mngelizuia kwa sababu ya kuhofu kuzitumia. Na mtu tangu hapo tabia yake ni mchoyo mno!"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Lau kuwa nyinyi mnazimiliki khazina za rehema za Mola wangu Mlezi, basi hapana shaka mngeli zuia kuzitumia kwa ajili ya kukhofu. Na mwanaadamu tangu hapo tabia yake ni mchoyo!. [100]

[100] Waambie hawa washirikina: Lau kuwa mnazimiliki riziki za Mola wangu Mlezi, mngeli zifanyia ubakhili kwa kuogopa ufakiri. Kwani ni tabia ya watu kuwa na pupa na ubakhili. Na Mwenyezi Mungu, Mkwasi na Karimu, humpa anacho taka amtakaye, na huteremsha miujiza aitakayo Yeye, sio waitakayo watu. Na Yeye katika yote hayo ni Mwenye hikima na Mjuzi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Lau nyinyi mngemiliki hazina za rehema za Mola wangu ambazo hazimaliziki wala hazitoweki, basi mungalizifanyia ubahili msitoe katika hizo kuwapa wengine kwa kuchelea zisimalizike mkawa mafukara.» Na ni katika tabia ya binadamu kuwa yeye ni mgumu wa kile kilicho mkononi mwake, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net