Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 101

Al-Israa 17:101

الإسراء

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَىٰ تِسْعَ ءَايَـٰتٍۭ بَيِّنَـٰتٍ ۖ فَسْـَٔلْ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ إِذْ جَآءَهُمْ فَقَالَ لَهُۥ فِرْعَوْنُ إِنِّى لَأَظُنُّكَ يَـٰمُوسَىٰ مَسْحُورًا

Maana

Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Basi waulize Wana wa Israili alipowafikia, na Firauni akamwaambia, "Hakika mimi ninakuona wewe Musa umerogwa!"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa!. [101]

[101] Na lau hawa watu wangeli letewa hizo ishara wazitakazo, wange zigeuzia uso, wala wasinge ziamini! Na Sisi tulimpa Musa Ishara tisa wazi. Na juu ya hivyo wakakufuru. Na Firauni akasema: Hakika mimi nakuona wewe, Musa, ni mtu uliye rogwa! Hizo ishara tisa ni: 1. Fimbo, 2. Mkono Mweupe, 3. Tufani, 4. Nzige na vyura na chawa na damu, 5. Ukame na upungufu wa mazao, 6. Kupasuka bahari, 7. Kutimbuka maji baharini, 8. Kuning'inia mlima kama kivuli, 9. Kusemezwa na Mola wake Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tulimpa Mûsã miujiza tisa iliyo waziwazi, yenye kutolea ushahidi wa ukweli wa unabii wake, nayo ni fimbo, mkono, ukame, upungufu wa matunda, mafuriko, nzige, chawa, vyura na damu. Basi waulize Mayahudi, ewe Mtume, suala la kuthibitisha, pale Mûsã alipowajia mababu zao na miujiza iliyo wazi, Fir‛awn akasema kumwambia Mûsã, «Mimi nadhani, ewe Mûsã, kwamba wewe ni mchawi uliodanganywa na kutekwa akili yako kwa vitendo hivyo vya ajabu unavyovileta».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net