Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 98

Al-Israa 17:98

الإسراء

ذَٰلِكَ جَزَآؤُهُم بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا وَقَالُوٓا۟ أَءِذَا كُنَّا عِظَـٰمًا وَرُفَـٰتًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا

Maana

Hayo ni malipo yao kwa sababu walizikataa ishara zetu, na wakasema: Hivyo tukishakuwa mifupa na mapande yaliyovurugika tutafufuliwa kwa umbo jipya?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni malipo yao kwa sababu walizikataa ishara zetu, na wakasema: Hivyo tukisha kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika tutafufuliwa kwa umbo jipya? [98]

[98] Adhabu hiyo ndiyo malipo yao kwa sababu ya kuzikataa dalili tulizo waletea za kuthibitisha Haki, na kwa ile kauli yao kusema: Hivyo sisi tutafufuliwa kwa umbo jipya baada ya kwisha kuwa mifupa na vumbi?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Adhabu hii iliyosifiwa ni mateso kwa washirikina kwa sababu ya kukanusha kwao aya za Allah Mtukufu na hoja Zake, kukanusha kwao Mitume Wake waliowaita kumuabudu Yeye na kule kusema kwao kwa njia ya kukataa, waamrishwapo kuamini kuwa kuna Ufufuzi, «Tutakapokufa na tukawa mifupa iliyochakaa na vipande vilivyotengeka mbalimbali, je tutafufuliwa baada yake hali ya kuwa ni viumbe vipya?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net