Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 97

Al-Israa 17:97

الإسراء

وَمَن يَهْدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِهِۦ ۖ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَّأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَـٰهُمْ سَعِيرًا

Maana

Na yule ambaye Mwenyezi Mungu anamuongoa, basi huyo ndiye aliyeongoka. Na yule ambaye anampotoa, basi hutawapatia walinzi wowote badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali ya kuwa wanakokotwa juu ya nyuso zao, huku ni vipofu, mabubu, na viziwi. Na makazi yao ni Jahannamu. Kila ukifanya kuzimika, tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na anaye mhidi (muongoza) Mwenyezi Mungu basi huyo ndiye aliye hidika. Na anaye wapotoa basi huto wapatia walinzi badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu na mabubu na viziwi. Na makaazi yao ni Jahannamu. Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu. [97]

[97] Waambie: Yule ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa kwa kuwa yu tayari kufuata uwongofu, basi huyo ni mwongofu. Na anaye mpotoa kwa kufisidika khulka yake, hutopata wa kuwanusuru asiye kuwa Yeye wa kuwaongoa duniani. Na Akhera tutawakusanya wakikokotwa juu ya nyuso zao, hawaoni, wala hawasemi, wala hawasikii. Na mahali pao wanapo pelekwa kukaa ni Jahannamu. Kula moto ukipungua ukali wake Mwenyezi Mungu anazidi kuuchochea uwake kwa nguvu zaidi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yoyote yule ambaye Allah Mtukufu atamuongoza ndiye mwenye kuongoka kwenye haki, na yoyote yule ambaye Yeye atampoteza, Akamdhalilisha na Akamuachia yeye na nafsi yake basi huyo hakuna mwenye kumuongoza badala ya Allah Mtukufu. Hawa wapotevu Allah Mtukufu Atawafufua Siku ya Kiyama na Awakusanye kwa nyuso zao hali wakiwa hawaoni wala hawatamki wala hawasikii. Mwisho wao ni moto wa Jahanamu wenye kuwaka, kila kutuliapo kuwaka kwake na kuzimika mroromo wake, tunawazidishia moto wenye kuwaka na kuroroma.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net