Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 96

Al-Israa 17:96

الإسراء

قُلْ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًۢا بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرًۢا بَصِيرًا

Maana

Sema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye ana habari zote za waja wake na anawaona vyema."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona. [96]

[96] Sema: Kama mnaukataa Utume wangu, basi Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutuhukumu baina yangu na nyinyi, akathibitisha ukweli wa Ujumbe wangu kwenu. Hakika Yeye kwa waja wake ni Mwenye kujua hali zenu, na Mwenye kuviona vitendo vyenu. Naye ni Mwenye kukulipeni kwa hivyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, «Inatosha kuwa Allah Mtukufu ni shahidi baina yangu mimi na nyinyi juu ya ukweli wangu na uhakika wa unabii wangu. Hakika Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mtambuzi wa hali za waja Wake ni Muoni wa matendo yao, na Atawalipa kwa hayo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net