Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 95

Al-Israa 17:95

الإسراء

قُل لَّوْ كَانَ فِى ٱلْأَرْضِ مَلَـٰٓئِكَةٌ يَمْشُونَ مُطْمَئِنِّينَ لَنَزَّلْنَا عَلَيْهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَلَكًا رَّسُولًا

Maana

Sema, "Ingelikuwa katika ardhi wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao, basi bila ya shaka tungeliwateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ingeli kuwa duniani wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao, basi bila ya shaka tungeli wateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao. [95]

[95] Sema kwa kuwarudi: Lau kuwa duniani badala ya wanaadamu wapo Malaika wanatembea kama wanaadamu na wamekaa humo, basi tungeli wateremshia kutoka mbinguni Malaika kuwa ni Mitume wao katika jinsi yao. Lakini Malaika si kama binaadamu; na wangeli kuja basi wange kuja kwa sura za watu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Muhammad, ukiwarudi washirikina kule kukanusha kwao kuwa Mtume ni miongoni mwa wanadamu, «Lau juu ya hii ardhi kungekua na Malaika wanatembea kwa kujituliza, tungaliwapelekea mtume miongoni mwa jinsi yao,» lakini watu wa ardhi ni wanadamu, basi mtume wa kupelekewa inatakiwa awe ni miongoni mwa jinsi yao, ili iwezekane kwao kuzungumza naye na kufahamu maneno yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net