Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 94

Al-Israa 17:94

الإسراء

وَمَا مَنَعَ ٱلنَّاسَ أَن يُؤْمِنُوٓا۟ إِذْ جَآءَهُمُ ٱلْهُدَىٰٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓا۟ أَبَعَثَ ٱللَّهُ بَشَرًا رَّسُولًا

Maana

Na hakikuwazuilia watu kuamini ulipowajia uongofu isipokuwa ni kwamba walisema, "Je, Mwenyezi Mungu alimtuma mtu kuwa ni Mtume?"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na nini kilicho wazuilia watu kuamini ulipo wajia uwongofu isipo kuwa walisema: Je! Mwenyezi Mungu humtuma mwanaadamu kuwa ni Mtume? [94]

[94] Na nini kilicho wazuilia washirikina wa Makka kuifuata Haki ulipo wajia wahyi (ufunuo) pamoja na miujiza isipo kuwa madai yao kwa ujinga wao ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hatumi Mitume wanaadamu, ila huwa ni Malaika!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakuna kilichowazuia makafiri kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na kuwatii, pindi ulipowajia wao ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa Allah Mtukufu, isipokuwa ni kule kusema kwao kwa ujinga na kwa njia ya kukanusha, «Je, kwani Allah Mtukufu ametuma Mtume miongoni mwa jinsi ya binadamu?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net