Al-Israa 17:93
الإسراءأَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِّن زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَىٰ فِى ٱلسَّمَآءِ وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَـٰبًا نَّقْرَؤُهُۥ ۗ قُلْ سُبْحَانَ رَبِّى هَلْ كُنتُ إِلَّا بَشَرًا رَّسُولًا
Au uwe na nyumba iliyopambwa, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako huko mpaka ututeremshie kitabu tukisome.ˮ Sema, “Subhana Rabbi (Ametakasika Mola wangu Mlezi)! Kwani mimi ni nani isipokuwa ni mtu tu Mtume?"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na Mtume? [93]
[93] Au uwe na nyumba iliyo pambwa kwa dhahabu, au upae mbinguni. Na hata hivyo hatukusadiki mpaka ukituletea kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha ukweli wako tukisome! Waambie: Mola wangu Mlezi ametakasika kabisa na kuhukumiwa na yeyote, au yeyote kushirikiana naye katika kudra yake! Mimi si chochote ila ni mwanaadamu kama Mitume wote wengineo. Na wala wao hawakuwaletea watu wao muujiza ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upande daraja za kukupaisha mbinguni, na hatutaamini kupaa kwako mpaka urudi ukiwa na kitabu kitokacho kwa Allah Mtukufu kilichofunguliwa tusome ndani yake kwamba wewe ni Mtume wa Allah Mtukufu kikweli.» Sema, ewe Mtume, kwa kushangaa juu ya ushindani wa makafiri hawa, «Kutakasika na sifa za upungufu ni kwa Mola wangu! Kwani mimi si chochote, isipokuwa ni mja miongoni mwa waja Wake mwenye kufikisha ujumbe Wake? Basi vipi mimi nitaweza kuyafanya mnayoyataka?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net