Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 67

Al-Israa 17:67

الإسراء

وَإِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فِى ٱلْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّآ إِيَّاهُ ۖ فَلَمَّا نَجَّىٰكُمْ إِلَى ٱلْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ ۚ وَكَانَ ٱلْإِنسَـٰنُ كَفُورًا

Maana

Na inapowakuta taabu katika bahari, hao mnaowaomba wanapotea, isipokuwa Yeye tu. Na anapowaokoa mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanadamu ni mwingi wa kukufuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnao waomba wanapotea, isipo kuwa Yeye tu. Na anapo kuvueni mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanaadamu ni mwingi wa kukanusha. [67]

[67] Mkisibiwa na madhara na mkakabiliwa na khatari katika bahari, hukukimbieni wote hao muwaombao kwa haja zenu isipo kuwa Mwenyezi Mungu peke yake. Kwani nyinyi hapo hamumkumbuki mwenginewe. Lakini akisha kuvueni na kuzama na akakufikisheni nchi kavu, mnaacha Tawhid, kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja, na mnakufuru neema. Ndio mtindo wa binaadamu daima kukataa neema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mkipatikana na shida baharini mkakaribia kuzama na kuangamia, wanapotea kwenye akili zenu wale waungu ambao mlikuwa mkiwaabudu, na mkamkumbuka Allah Mtukufu Muweza, Peke Yake, Awasaidie na Awaokoe, hapo mnamtakasia katika kutaka msaada na uokozi, na Yeye Anawasaidia na Anawaokoa. Anapowaokoa kwa kuwafikisha kwenye nchi kavu, mnageuka mkaacha Imani, kumtakasia Allah Mtukufu na matendo mema. Na huu ni katika ujinga wa binadamu na ukafiri wake, kwani binadamu ni mkanushaji sana neema za Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net