Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 66

Al-Israa 17:66

الإسراء

رَّبُّكُمُ ٱلَّذِى يُزْجِى لَكُمُ ٱلْفُلْكَ فِى ٱلْبَحْرِ لِتَبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِهِۦٓ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا

Maana

Mola wenu Mlezi ndiye anayewaendeshea merikebu katika bahari ili mtafute katika fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwingi wa kukurehemuni.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wenu Mlezi ndiye anaye kuendesheeni marikebu katika bahari ili mtafute katika fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kukurehemuni nyinyi. [66]

[66] Mola wenu Mlezi ni Yeye peke yake ndiye anaye ziendesha marikebu baharini ambazo kwazo nyinyi mnatafutia manufaa kwa biashara na mengineyo. Yeye daima ni Mwenye rehema kwenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mola wenu, enyi watu, Ndiye Anayewaendeshea vyombo vya kusafiria baharini ili mtafute riziki ya Allah Mtukufu katika safari zenu na biashara zenu. Hakika Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mwingi wa huruma kwa waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net