Al-Israa 17:65
الإسراءإِنَّ عِبَادِى لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَـٰنٌ ۚ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ وَكِيلًا
Hakika wewe huna mamlaka yoyote juu ya waja wangu. Na Mola wako Mlezi anatosha kuwa ni Mtegemewa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wewe huna mamlaka juu ya waja wangu. Na Mola wako Mlezi anatosha kuwa ni wa kutegemewa. [65]
[65] Ama waja wangu walio nisafia niya Mimi wewe huna uwezo wa kuwapotoa, kwa kuwa wao wanamtegemea Mola wao Mlezi. Na Yeye anatosha kabisa kuwa ni wa kuwanusuru wakimtaka msaada wa kusalimika nawe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Hakika waja wangu Waumini waliotakaswa ambao walinitii, wewe huna uwezo wa kuwapoteza.» Na inatosha kuwa Mola wako, ewe Mtume, kuwa Ndiye Mwenye kuwalinda na kuwahifadhi Waumini kutokana na vitimbi vya Shetani na udanganyifu wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net