Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 64

Al-Israa 17:64

الإسراء

وَٱسْتَفْزِزْ مَنِ ٱسْتَطَعْتَ مِنْهُم بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِى ٱلْأَمْوَٰلِ وَٱلْأَوْلَـٰدِ وَعِدْهُمْ ۚ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ إِلَّا غُرُورًا

Maana

Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na Shetani hawapi ahadi isipokuwa ya udanganyifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na Shet'ani hawapi ahadi ila ya udanganyifu. [64]

[64] Na wazuge na wavute kwa kuwaita wamuasi Mwenyezi Mungu hao unao waweza miongoni mwao. Na fanya kila juhudi yako ya namna zote za udanganyifu. Na shirikiana nao katika kuchuma mali ya haramu, na kuyatumia kwa haramu, na kuwakufurisha watoto na kuwaghuri wafanye fisadi. Na wape ahadi za uwongo, kama kuwa miungu yao itawaombea, na kuwa watapata utukufu kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya nasaba zao. Na Shetani hawaahidi wafwasi wake ila kwa udanganyifu na uficho.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na uwalaghai wale unaoweza kuwalaghai miongoni mwao kwa kuwaita kuniasi, na uwakusanyie askari zako unaowaweza, kati ya kila aliye juu ya kipando na anayetembea kwa miguu, na ujishirikishe nao katika mali yao wanayoyachuma kwa njia za haramu, na ujishirikishe nao katika watoto wao kwa kuwapambia uzinifu na uasi na kwenda kinyume na maamrisho ya Allah Mtukufu mpaka uenee uchafu na uharibifu, na uwaahidi wafuasi wako, miongoni mwa wale wanaozalikana na Ãdam, ahadi za urongo, na kila ahadi za Shetani ni ubatilifu na udanganyifu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net