Al-Israa 17:63
الإسراءقَالَ ٱذْهَبْ فَمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَآؤُكُمْ جَزَآءً مَّوْفُورًا
Akasema Mwenyezi Mungu: Nenda! Na atakayekufuata katika wao, basi hakika Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yenu, malipo yaliyo mengi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema Mwenyezi Mungu: Ondokelea mbali! Atakaye kufuata katika wao, basi Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yenu, malipo ya kutimia. [63]
[63] Mola akamwambia kwa kumtisha na kumlegezea kamba: Endelea na shani yako uliyo jichagulia kuifuata. Atakaye kut'ii wewe katika wana wa Adam, basi Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yako na yao, malipo ya kutosha yaliyo kamilika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Aliyetukuka Akasema Akimuonya Iblisi na wafuasi wake, Nenda! Yoyote mwenye kukufuata miongoni mwa kizazi cha Ãdam, basi mateso yako na mateso yao ndani ya moto wa Jahanamu ni mengi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net