Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 62

Al-Israa 17:62

الإسراء

قَالَ أَرَءَيْتَكَ هَـٰذَا ٱلَّذِى كَرَّمْتَ عَلَىَّ لَئِنْ أَخَّرْتَنِ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ لَأَحْتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُۥٓ إِلَّا قَلِيلًا

Maana

Akasema, "Hebu unamuona huyu uliyemtukuza zaidi yangu, ukiniahirisha mpaka Siku ya Kiyama, hapana shaka nitakiangamiza kizazi chake isipokuwa wachache tu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Hebu nambie khabari ya huyu uliye mtukuza juu yangu. Ukiniakhirisha mpaka Siku ya Kiyama, hapana shaka nitawaangamiza dhuriya zake wasipo kuwa wachache tu. [62]

[62] Iblisi akasema: Ewe Mola wangu Mlezi hebu ni ambie khabari za huyu uliye mtukuza juu yangu, ukaniamrisha ni msujudie kwanini kamtukuza kuliko mimi, na mimi ni bora kuliko yeye, Naapa kwa utukufu wako. Ukinibakisha ni hai mpaka siku ya Kiyama, basi nitawahiliki dhuria zao watao wazaa kwa kuwaghuri isipokwa wachache tu, kati yao utakao walinda na Kuwahifadhi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Iblisi akasema akionesha ujasiri wake na ukafiri kwa Allah Mtukufu, «Unamuona kiumbe huyu uliyemfadhilisha juu yangu? Ukinibakisha hai mpaka Siku ya Kiyama nitawatawala wale wanaozalikana na yeye kwa kuwapoteza na kuwaharibu isipokuwa wale waliotakaswa katika Imani, nao ni wachache».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net