Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 61

Al-Israa 17:61

الإسراء

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِـَٔادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ قَالَ ءَأَسْجُدُ لِمَنْ خَلَقْتَ طِينًا

Maana

Na pale tulipowaambia Malaika, "Msujudieni Adam." Wakamsujudia isipokuwa Iblisi. Akasema, "Je, nimsujudie uliyemuumba kwa udongo?"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam. Wakamsujudia isipo kuwa Iblisi. Akasema: Je! Nimsujudie uliye muumba kwa udongo? [61]

[61] Na Mwenyezi Mungu anakumbusha asli ya kuumba na uadui baina ya mwanaadamu na Iblisi, pale alipo waambia Malaika: Msujudieni Adam kwa kumuamkia na kumhishimu kwa kumuinamia. Hapo hapo wakasujudu. Isipo kuwa Iblisi akakataa, na akasema kwa chuki: Vipi nimsujudie uliye muumba kwa udongo, na hali mimi umeniumba kwa moto. Mimi ni bora kuliko yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ukumbuke neno tulilowaambia Malaika wamsujudie Ãdam kwa kumwamkia na kumheshimu, wakamsujudia wote isipokuwa Iblisi, alifanya kiburi na akakataa kusujudu, na huku akisema kwa njia ya kupinga na kujiona, «Je, nimsujudie huyu dhaifu aliyeumbwa kwa udongo?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net