Al-Israa 17:60
الإسراءوَإِذْ قُلْنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِٱلنَّاسِ ۚ وَمَا جَعَلْنَا ٱلرُّءْيَا ٱلَّتِىٓ أَرَيْنَـٰكَ إِلَّا فِتْنَةً لِّلنَّاسِ وَٱلشَّجَرَةَ ٱلْمَلْعُونَةَ فِى ٱلْقُرْءَانِ ۚ وَنُخَوِّفُهُمْ فَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا طُغْيَـٰنًا كَبِيرًا
Na tulipokwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwishawazingira hao watu. Na hatukuifanya ndoto tuliyokuonyesha isipokuwa ni kuwajaribu watu, na mti uliolaaniwa katika Qur-ani. Na tunawahofisha, lakini haiwazidishii isipokuwa uasi mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tulipo kwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwisha wazunguka hao watu. Na hatukuifanya ndoto tulio kuonyesha ila ni kuwajaribu watu, na mti ulio laaniwa katika Qur'ani. Na tunawahadharisha, lakini haiwazidishii ila uasi mkubwa. [60]
[60] Ewe Nabii! Kumbuka tulipo kwambia: Hakika Mola wako Mlezi amewazunguka hao watu. Wao wamo wamedhibitiwa na kudra yake. Basi wewe wafikishie Ujumbe wala usimwogope yeyote katika wao. Mwenyezi Mungu atakulinda nao. Na mambo ya ajabu uliyo yaona katika Usiku wa Israi (Safari ya Usiku), hatukuyafanya Sisi ila yawe ni mtihani na majaribio kwa wanaadamu. Kwa hayo ipate kuzidi Imani ya Muumini, na ukafiri wa kafiri. Na wala hatukuufanya ule mti ulio subiwa katika Qur'ani, nao ni Mti wa Zaquum, unao mea huko Motoni, isipo kuwa ni kuwafanyia wao pia mtihani pale walipo sema: Moto unaunguza mti, basi vipi mti umee katika moto? Pia ni kuzidi kuwahadharisha kwa hayo. Lakini kuwahadharisha kwetu hakuwazidishii isipo kuwa kupindukia kiwango kikubwa kabisa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipokwambia kwamba Mola wako Amewazunguka watu kwa ujuzi na uwezo. Na hatukuijaalia ndoto tuliyokuonyesha waziwazi usiku wa isrã’ (kwenda Bayt al-Maqdis) na mi‛rãj (kupaa kwenda mbinguni) miongoni mwa maajabu ya viumbe isipokuwa ni kuwatahini watu. Na tunawatisha washirikina kwa aina mbalimbali za adhabu na miujiza, lakini kuwatisha huko hakuwaongezei isipokuwa ni kuendelea zaidi kwenye ukafiri na upotevu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net