Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 59

Al-Israa 17:59

الإسراء

وَمَا مَنَعَنَآ أَن نُّرْسِلَ بِٱلْـَٔايَـٰتِ إِلَّآ أَن كَذَّبَ بِهَا ٱلْأَوَّلُونَ ۚ وَءَاتَيْنَا ثَمُودَ ٱلنَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا۟ بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِٱلْـَٔايَـٰتِ إِلَّا تَخْوِيفًا

Maana

Na hakuna kinachotuzuia kutuma miujiza ila ni kuwa watu wa zamani waliikanusha. Na tuliwapa Wathamudi ngamia jike kuwa ni Ishara iliyo dhaahiri, lakini walidhulumu kwaye. Nasi hatutumii Ishara isipokuwa kwa ajili ya kuhofisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hapana kinacho tuzuia kupeleka miujiza ila ni kuwa watu wa zamani waliikanusha. Na tuliwapa Wathamudi ngamia jike kuwa ni Ishara iliyo dhaahiri, lakini walidhulumu kwaye. Nasi hatupeleki Ishara ila kwa ajili ya kuhadharisha. [59]

[59] Watu wako wamekutaka uwaletee Ishara na miujiza. Nao hawakukinaika kwa yaliyo wajia ambayo huwakinaisha wenye akili. Na mwendo wetu umekwisha wapitia hao wanao taka miujiza, na wanapo kubaliwa wasiamini, nao ni kuwang'olea mbali kwa adhabu kama tulivyo wafanyia wa kale. Miongoni mwa hao ni watu wa Thamud. Walitaka miujiza, akawa ngamia mke ni muujiza wazi kwao wa kuondoa shaka zote. Wakamkanusha, yakatokea kwao yaliyo tokea! Na imekuwa hikima ya Mwenyezi Mungu kuwa asiwakubalie hayo waliyo yataka, kwa kuchelea wasiikatae miujiza, kwa kutarajia watakuja amini miongoni mwao, au watakuja zaa watakao amini. Na miujiza hakika Sisi huwapelekea watu kwa kuwatia khofu na kitisho.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakuna kilichotuzuia kuteremsha miujiza ambayo washirikina waliitaka isipokuwa ni kwamba ummah waliowatangulia waliikanusha, Allah Mtukufu Aliwajibu kwa waliyotaka wakakanusha na wakaangamia. Na tuliwapa Thamûd, nao ni watu wa Ṣãlih, miujiza iliyo wazi, nayo ni ngamia, wakaikanusha na tukawaangamiza. Na huku kutuma kwetu Mitume wakiwa na alama, mazingatio na miujiza tuliyoipitisha kwenye mikono yao, hakukuwa isipokuwa ni kuwatisha waja wapate kuzingatia na wakumbuke.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net