Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 58

Al-Israa 17:58

الإسراء

وَإِن مِّن قَرْيَةٍ إِلَّا نَحْنُ مُهْلِكُوهَا قَبْلَ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ أَوْ مُعَذِّبُوهَا عَذَابًا شَدِيدًا ۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِى ٱلْكِتَـٰبِ مَسْطُورًا

Maana

Na hakuna mji wowote ila Sisi tutauteketeza kabla ya Siku ya Kiyama, au tutaupa adhabu kali. Haya yamekwishaandikwa katika Kitabu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hapana mji wowote ila Sisi tutauteketeza kabla ya Siku ya Kiyama, au tutaupa adhabu kali. Haya yamekwisha andikwa katika Kitabu. [58]

[58] Na ni mazoea yetu kuuteketeza kila mji na watu wake unapo dhulumu mji huo. Au huwapa adhabu kali watu wake kwa mauwaji au vyenginevyo. Basi watu wako watahadhari, kwani hukumu yetu imekwisha hukumiwa, na imekwisha andikwa katika Kitabu chetu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Anawaonya wanaokufuru kwamba hakuna mji wowote wenye kukufuru na kukanusha Mitume isipokuwa mateso Yake yataushukia kwa maangamivu hapa duniani kabla ya Siku ya Kiyama au kwa adhabu kali juu ya watu wake. Hayo ni maandishi Aliyoyaandika Allah Mtukufu na hukumu Aliyoipitisha, hapana budi kujiri, nayo imeandikwa kwenye Al-Lawḥ Al- Mahfûḍ (Ubao Uliohifadhiwa).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net