Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 57

Al-Israa 17:57

الإسراء

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ ٱلْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُۥ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُۥٓ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا

Maana

Hao ambao wao wanawaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi hata miongoni mwao walio karibu mno, na wanataraji rehema zake, na wanaihofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhariwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo. [57]

[57] Na hakika hawa viumbe wanao waomba wale wanao waabudu, wao wenyewe wanamuabudu Mwenyezi Mungu, na wanaomba wapate daraja na cheo kwake kwa ut'iifu, na wana pupa ya kutaka wawe karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, na wanatumaini kupata kwake rehema, na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mwenyezi Mungu inatakikana kutahadhari nayo na kuiogopa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao ambao washirikina wanawaomba, miongoni mwa Manabii, watu wema na Malaika, wao wenyewe wanashindana kujiweka karibu na Mola wao kwa matendo mema wanayoyaweza, wanatarajia rehema Yake na wanaogopa adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako ndiyo ambayo inatakikana kwa waja wawe na hadhari nayo na waiogope.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net