Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 56

Al-Israa 17:56

الإسراء

قُلِ ٱدْعُوا۟ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِۦ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ ٱلضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا

Maana

Sema: Waombeni hao mnaowadai badala yake Yeye. Hawawezi kuwaondolea madhara, wala kuyaweka pengine.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Waombeni hao mnao wadaia badala yake Yeye. Hawawezi kukuondoleeni madhara, wala kuyaweka pengine. [56]

[56] Waambie hawa wanao abudu viumbe na wanadai kuwa hao ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu: Waombeni hao mnao waabudu inapo kuteremkieni shida, au mkakhofu kuwa itakushukieni. Hamtopata kwao chochote cha kukuondoleeni madhara yenu, wala kuyahamisha akapewa mwinginewe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina wa Makkah, «Hawa masanamu mnaowaita wawaondolee shida hawawezi hilo wala hawawezi kuiepusha kwenu nyinyi kuipeleka kwa wengine, na pia hawawezi kuigeuza kutoka namna ilivyo kuifanya namna nyingine, Mwenye kuweza hilo ni Allah Mtukufu Peke Yake.» Aya hii inakusanya kila anayeombwa asiyekuwa Allah Mtukufu, miongoni mwa Manabii, watu wema na wasiokuwa hao, kwa tamko la istighãthah (kutaka uokozi) au du‛a’ (maombi) au mfano wake, kwani hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net