Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 55

Al-Israa 17:55

الإسراء

وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِمَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ عَلَىٰ بَعْضٍ ۖ وَءَاتَيْنَا دَاوُۥدَ زَبُورًا

Maana

Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine, na Daudi tulimpa Zaburi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa Zaburi. [55]

[55] Na Mola wako Mlezi anajua vilivyo vyote viliomo mbinguni na ardhini, na anajua hali zao. Basi anawakhiari miongoni mwao kwa kuwapa Unabii awatakao. Naye amekukhiari wewe kwa kukupa Utume wake. Basi haiwafalii wao kuudhika na Unabii wako. Na hao Manabii si wote sawa sawa kwa daraja mbele yake Aliye tukuka shani yake. Bali baadhi yao ni bora kuliko wenginewe. Naye amewatukuza baadhi ya Manabii juu ya wengine kwa miujiza, na wingi wa wafwasi, si kwa ufalme. Basi alitukuzwa Daudi kwa kuwa kapewa Zaburi, si kwa kuwa kapewa ufalme. Basi hapana ajabu kuwa wewe, Muhammad, ukapata fadhila kubwa kabisa kwa kuwa umepewa Qur'ani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Mola wako, ewe Mtume, Anawajua zaidi walioko mbinguni na ardhini, na tumewafadhilisha baadhi ya Mitume juu ya wengine kwa matukufu, wingi wa wafuasi na kuwateremshia Vitabu, na Dãwûd, amani imshukie, tumempa Zaburi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net