Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 54

Al-Israa 17:54

الإسراء

رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِكُمْ ۖ إِن يَشَأْ يَرْحَمْكُمْ أَوْ إِن يَشَأْ يُعَذِّبْكُمْ ۚ وَمَآ أَرْسَلْنَـٰكَ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا

Maana

Mola wenu Mlezi anawajua vilivyo. Akitaka, atawarehemu, na akitaka, atawaadhibu. Na hatukukutuma ili uwe msimamizi wao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wenu Mlezi anakujueni vilivyo. Akipenda atakurehemuni, na akipenda atakuadhibuni. Na hatukukutuma ili uwe mlinzi juu yao. [54]

[54] Mola wenu Mlezi ndiye anaye jua vyema mwisho wa mambo yenu. Akipenda atakurehemuni kwa kukupeni tawfiki ya Imani, (uwezo wa kuamini) au akipenda atakupeni adhabu kwa kuikosa hiyo Imani. Wala Sisi hatukukupeleka wewe uwe ni mwakilishi wao kwa mambo yao, hata uwalazimishe kuamini. Bali tumekutuma uwe ni mbashiri kuwapa khabari njema wenye kusadiki, na mwonyaji kuwaonya wanao kanusha. Waachilie mbali, na waamrishe sahaba zako wawastahamilie.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mola wenu Anawajua nyinyi zaidi, enyi watu, Akitaka Atawarehemu Awaafikie kwenye Imani au Akitaka atawafisha kwenye ukafiri kisha Awaadhibu. Na hatukukutumiliza, ewe Mtume, uwe ni muwakilishi juu yao, unayapanga mambo yao na unawalipa kwa matendo yao, jukumu lako ni kuyafikisha uliyotumilizwa kwayo na kuieleza njia iliyonyooka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net