Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 53

Al-Israa 17:53

الإسراء

وَقُل لِّعِبَادِى يَقُولُوا۟ ٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ ٱلشَّيْطَـٰنَ يَنزَغُ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ ٱلشَّيْطَـٰنَ كَانَ لِلْإِنسَـٰنِ عَدُوًّا مُّبِينًا

Maana

Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, kwa maana hakika Shetani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shetani ni adui aliye dhahiri kwa mwanadamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maana Shet'ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu. [53]

[53] Ewe Nabii! Waambie waja wangu Waumini wanapo pambana na washirikina waseme maneno yaliyo bora ya kukinaisha, na waachilie mbali kutumia maneno makali makali yanayo sabibisha shari na uharibifu. Kwani Shetani huleta fisadi baina ya Waumini na makafiri, kwa kuwa yeye ni adui aliye wazi wa binaadamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na waambie waja wangu Waumini waseme, katika mazungumzo yao na kushauriana kwao wao kwa wao, maneno mazuri, kwani wao wakitofanya hivyo Shetani atatia ugomvi, uharibifu na utesi baina yao. Hakika Shetani kwa binadamu ni adui aliyeudhihirisha uadui.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net