Al-Israa 17:52
الإسراءيَوْمَ يَدْعُوكُمْ فَتَسْتَجِيبُونَ بِحَمْدِهِۦ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا
Siku atakapowaita, nanyi mtamuitikia kwa kumsifu, na mtadhani kuwa hamkukaa isipokuwa muda mdogo tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
iku atakapo kuiteni, na nyinyi mkamuitikia kwa kumshukuru, na mkadhani kuwa hamkukaa ila muda mdogo tu. [52]
[52] Na siku atapo kufufueni Mwenyezi Mungu kutoka makaburini kwenu, mtafufuliwa nanyi mkimshukuru na kumsifu Mola wenu Mlezi kwa ukamilifu wa uwezo wake. Na mtadhani kuwa hamkukaa makaburni kwenu ila muda mchache tu. Mtaona muda ni mfupi kwa mnasaba ya hayo mnayo yaendea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Siku Atakapowaita Muumba wenu mtoke kwenye makaburi yenu na mkaitika amri ya Allah Mtukufu na mkaifuata, na shukrani ni Zake kwa kila namna, na mkadhani, kwa kitisho cha Siku ya Kiyama na kwa kipindi kirefu cha kukaa kwenu Akhera, kwamba nyinyi hamkukaa duniani isipokuwa muda mchache.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net