Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 51

Al-Israa 17:51

الإسراء

أَوْ خَلْقًا مِّمَّا يَكْبُرُ فِى صُدُورِكُمْ ۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَا ۖ قُلِ ٱلَّذِى فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَ ۖ قُلْ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَرِيبًا

Maana

Au umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Ni nani atakayeturudisha tena? Sema: Yule yule aliyewaumba mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Ni lini hayo? Sema: Labda huenda itakuwa hivi karibuni!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au umbo lolote mnalo liona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Nani atakaye turudisha tena? Sema: Yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu! [51]

[51] Au umbo jingenelo lolote ambalo mnaona kwa mawazo yenu haliwezi kuwa hai, basi hapana shaka yoyote mtafufuliwa! Watasema kwa kuona ni muhali: Nani atakaye turejesha hivyo? Waambie: Atakurjesheeni Mwenyezi Mungu, yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza. Watakutikisia vichwa vyao kwa mastaajabu, nao wakisema kwa kejeli: Huko kufufuliwa unako tuahidi kutakuwa lini? Waambie: Nataraji kutakuwa karibu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au kuweni umbo lolote kubwa ambalo akili zenu zaliona kuwa liko mbali na uhakika. Na watasema kwa kukanusha, «Ni nani atakayeturudisha kwenye uhai baada ya kufa?» Waambie, «Atakayewarudisha na kuwarejesha ni Allah Mtukufu Aliyewaumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako mara ya kwanza.» Na wasikiapo majibu haya watatikisa vichwa vyao kwa njia ya shere, huku wakiona ajabu na watasema, wakiliona jambo hilo kuwa ni mbali kukubalika, «Ufufuzi huu utatokea lini?» Sema, «Ni lipi linalowajulisha kwamba Ufufuzi huu, mnaoukanusha na mnaouona kuwa uko mbali, huenda ukawa ni wenye kutokea kipindi cha karibu?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net