Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 17 · Aya ya 68

Al-Israa 17:68

الإسراء

أَفَأَمِنتُمْ أَن يَخْسِفَ بِكُمْ جَانِبَ ٱلْبَرِّ أَوْ يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ثُمَّ لَا تَجِدُوا۟ لَكُمْ وَكِيلًا

Maana

Je, mna amani ya kuwa hatawadidimiza katika upande wowote katika nchi kavu, au kwamba hatawatumia tufani la kokoto? Kisha msipate yeyote wa kumtegemea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Mmeaminisha ya kuwa hatakudidimizeni upande wowote katika nchi kavu, au kwamba hatakuleteeni tufani la kokoto? Kisha msipate wa kumtegemea. [68]

[68] Na hapo tukisha kuvueni mkafika nchi kavu, kwani ndio mmeaminisha kuwa basi haikupateni adhabu ya Mwenyezi Mungu? Hasha! Akitaka anaweza akaipindua ardhi ikakuteketezeni chini yake. Na akitaka atakupelekeeni upepo mkali ukutupieni kokoto na mawe, na wala msipate wa kukulindeni na yanayo kupateni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, mumeghafilika, enyi watu, na adhabu ya Allah Mtukufu, ndipo mkajiaminisha kwamba ardhi haitawaporomokea ikawadidimiza au kwamba Allah Mtukufu Hatawanyesheza mvua ya mawe itokayo juu iwaue kisha msipate yoyote wa kuwalinda na adhabu Yake?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Israa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net